Katika mtaa mmoja katika Manispaa ya Dodoma kwenye Studio Mtaa wa Komba' 'Market' nilikuwa naegesha pikipiki yangu karibu na Studio hiyo Ghafla akaja mpiga picha mmoja akanikabidhi picha hiyo,jina nimelihifadhi akanidhihaki kuwa kumbe Mzee bado wamo. Nikamuuliza kwa nini? akasema nilidhani umestaafu kazi huwezi sasa hata kusukuma pikipiki.
Nilicheka sana nikamuambia alisikia wapi mtu akisataafu kazi ndiyo hawezi kila kitu ni nani." Sawa Mzee karibu Dodoma umetuacha na umetukuta kalamu na sisi,sisi na kalamu" alisema Bwana huyo.Na huyo alikuwa mwana habari.Na alikuwa akitambua mwana habari hastaafu ,bali atastaafu majukumu ya Utumishi wa Umma katika Habari.lakini kwenye Blog yangu hadi ninaposhindwa kuandika kabisa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni