Ijumaa, 20 Novemba 2015

RAIS JOHN POMBE MAGUFULI AMETAJA BAADHI YA KIRO ZITAKAZO TATULIWA NA SERIKALI YA AWAMU YA TANO ILI KUTEKELEZA AHADI WAKATI WA KUOMBA RIDHAA YA KUIONGOZA NCHI, AMESEMA HAYO WAKATI AKIFUNGUA BUNGE LA 11 MJINI DODOMA LEO

 Rais Dkt John Pombe Magufuli akihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dodoma leo
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Kassim akiapa katika viwanja vya Ikulu ndogo Chamwino nje ya mji wa Dodoma leo saa 4.asubuhi.
Mhe. Majaliwa akimshukuru Rais na wabunge wenzake  baada ya kuthibitishwa na wabunge wenzake hapo jana.

Dkt Magufuli ametaja baadhi ya kero hizo ni pamoja na Rushwa na ufisadi ambao unafanywa na baadhi ya watu waliopewa dhamana ya kuwahudumia wananchi katika sekta za Ardhi,Bandari,TAMISEMI, Maji safi na salama,TRA, TANESCO, na  Afya kuwa na lugha chafu kwa wagonjwa  pamoja na madawa kutokuwepo katika hospitali.
Kero nyingine ni pamoja na Ajira,Elimu,Vyombo ya usalama ,Polisi,mizani ya magari,Mahakam,Migodi hasa wachimbaji wadogo wadogo,madeni,kilimo, uvuvi na ufugaji pamoja na uchakavu wa miundo mbinu na ujenzi wa Reli za zamani na mpya.
Aidha alisema kuwa Serikali yake ya Awamu ya tano kuwa itatekelza ahadi zote zilizo ahidiwa za kuwa letea wananchi maendeleo kwa kujenga na kufufua viwanda  na wale ambao hawviendelezi serikali itavichukua.na kwamba kupitia Sekta binafsi inakuwa ni msingi imara ya kuleta maendeleo.
Alisema serikali hiyo itaimarisha ufuatiliaji,kilimo,mifugo na uvuvi,Viwanda vitapata mali ghafi kutoka ndani kwenye viwanda vya nguo ,mafuta,viatu.ili mafanikio katika kilimo wakulima wapatiwe zana za kisasa,kukopeshwa pamoja na kuondoa kodi katika mazao
Pia alisema kuwa akina mama lishe,bodaboda,wachimbaji wadogo wadogo wanufaike na Halmashauri,Wilaya, Mkoa kwa ushirikiano wao waondoe ushuru usiyo na sababu ili kuwa na ajira yao ya uhakika.
Katika kutekeleza ahadi zake Rais huyo amesema ataunda Mahakama ya Mafisadi na Rushwa,kwa chukizwa na rushwa na ufisadi amefananisha na mtumbua majipu.Ameomba ushirikiano kwa wabunge na wananchi afanye kazi ya kutumbua majipu hayo
Sambamba na hayo Rais amesitisha safari zote za nje ya nchi zikiwamo za mafunzo,badala yake ni rahisi kumwalika mkufunzi mmoja wa mafunzo hayo kuja kutoa mafunzo hapahapa nchini ili kuokoa fedha ambazo zingeweza kufanyia maendeleo katika Sekta za kijamii.
Amesema kuna watu wanapenda kusafiri kwenda nje kuliko kwenda kwao kusalimia wazazi wao ,ambapo kwa mwaka 2013/2014 safari za nje ya nchi zimegharimu shilingi Bilioni 356.324 ikiwa Gharama ya ticket ni billion 183.16,mafunzo billion 68.612 na posho shilingi bilioni.104.552 .
Waliotumia fedha hizo ni pamoja na Bunge,TAMISEMI,Mambo ya nje,fedha,ukaguzi na mambo mengine, hasa hasa anasisitiza uwajibikaji katika kubana matumizi ya fedha na hizo  pesa zinazokusanywa zitumike kwa maendeleo ya nchi.Kutokana na hayo alisema kuwa kuanzia januari 2016 elimu ni bure kutoaka Awali hadi Sekondari.
Kuona Rais huyo kuona umuhimu wa wananchi wake wanopata shida katika Sekta ya afya amesema fedha kiasi zaidi ya shilingi 230,000,000 rilizo kusanywa na wadau mablimbali  katika viwanja vya Bunge Mjini Dodoma kwenye hafla fupi aliyo iandaa Rais  zielekezwe kununulua vitanda vya hospitali
Na katika hotuba yake alifungua bunge la 11,ambapo Waziri Mkuu Majiliwa Kassim Majaliwa aliahirisha bune hilo hadi tarehe 26 Januari 2016,baada ya hotuba fupi kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Aidha ali ahidi kushirikiana na wabunge wote bila kujali Itikadi za Vyama baada ya hushuhudia wabunge wa Kambi ya upinzani kukaidi amri ya Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai na kuwa toa nje ya Bunge,si kitendo kizuri kwa wananchi walio wachagua kwenda kuwa wawakilisha 

Alhamisi, 19 Novemba 2015

MHESHIMIWA MAJALIWA KASSIM MAJALIWA ATHIBITISHWA KUWA WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WA AWAMU YA TANAO KWA ASILIMIA 73.5 KWA KURA 258 BAADA YA KUPIGIWA KURA NA WABUNGE WOTE LILIPO PELEKWA BUNGENI JINA LAKE KWA STAHILI YA AINA YAKE KUTOKA KWA RAIS.


Mheshimiwa Majiliwa amesemwa kuwa ni mtu, Mwadilifu,asiye na makundi, hana kashfa, mtetezi, mfuatiliaji, makini,msikivu, mwenye busara,ni mchapa kazi,kujichanganya na watu na mwana michezo,na kwamba ni kijana ambaye atatekeleza vyema moto wa hapa kazi tu kwaushirikiano na Rais ,wabunge wenzake pamoja na wananchi.
Majaliwa ni Waziri Mkuu kijana kati ya mawaziri wakuu wa Awamu zote ,aidha amewahi kufanya kazi mbalimbali zikiwemo kwenye Sekta ya elimu, akiwa mwalimu, Mkufunzi katika vyuo vya Ualimu, Katibu wa Chama Cha Walimu Tanzania, Mkuu wa Wilaya ,Naibu Waziri wa Elimu TAMISEMI.Akaibuka kwa kura 258 sawa na asilimia73.5
Kutokana na nafasi aliyokuwa nayo TAMISEMI na nyingine zote alizozifanya katika  Utumishi wake ,inasemakana ana upeo mkubwa wa kutekeleza majukumu yake kama Waziri Mkuu kwa kuwa anayaelewa vizuri maeneo yake atakayo yafanyia kazi bila mashaka yoyote. Kesho saa 4. Asubuhi ataapishwa katika viwanja vya Ikulu ndogo Chamwino Mjini Dodoma.
Hatimaye  Dkt Tulia ckson Mwansasu  akaibuka kuwa mshindi wa kiti cha Unaibu Spika kwa asilimia 71.2 sawa na kura 250 alizopata baada ya kumshinda Mhe.Magdalena Sakaya wa  CUF Kaliua Tabora aliyepata kura 101 sawa na asilimia 28.8.,nakwamba Dkt Mwansasu akaapishwa kuwa Naibu Spika wa Bunge la 11.
Hii ni Serikali ya kihistoria nchini Tanzania kuwa  na Rais  na Makamu wake mwanamke Mhe.Samia Suluhu Hassan na Naibu Sipika Bunge la Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania mwanamke Dkt Tulia Ackson Mwansasu. Kweli hapa ni kazi tu.kinacho hitajika ni ushirikiano kutoka kwa wananchi  wote.

Jumapili, 15 Novemba 2015

KAMATI KUU YA CCM KUTEUA MAJINA MATATU YA USPIKA WA BUNGE LA 11, MAJINA HAYO KUPIGIWA KURA NA KAMATI YA WABUNGE WOTE WA CCM LEO WHITE HOUSE DODOMA

Hayo yamesemwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye kwa waandishi wa Habari kuwa walio teuliwa kuwa ni pamoja na Naibu Spika wa Bunge la 10  Mhe. Job Ndugai, Mbunge wa Bunge la Afrika mashariki Mhe. Abdulla Mwinyi na Naibu mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Tulia Ackson.

Nnauye alisema majina hayo  yatapelekwa kupigiwa kura katika kikao cha Kamati ya wabunge wa CCM wote " White House"  majira ya asubuhu kuanzia saa 4. leo.


Kuhusu Naibu Sipika Nnauye aliseama atakayetaka uingia katika kuwania unaibu Spika atajaza fomu  ya maombi kwa ada ya sh. 100,000 kwa Katibu wa kamati ya wabunge wote wa CCM.Ataye ibuka mshindi tutakujuza baadae.

Alhamisi, 5 Novemba 2015

DKT. JOHN JOSEPH POMBE MAGUFULI AAPISHWA RASMI KUWA RAIS WA AWAMU YA TANO WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA MAKAMU WAKE MHE.SAMIA HASSAN SULUH NA JAJI MKUU WA TANZANIA MHE. OTHMAN CHANDE KATIKA UWANJA WA UHURU JIJINI DAR ES SALAAM,NA KUWASHUKURU WOTE WALIYO FANIKISHA KUWA RAIS

 Rais Mteule Dkt John Josehp Pombe Magufulu akiapa mbele ya Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe.Othman Chande katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dar es Salaam leo
 Makmu wa Rais Mhe. Samia Hassan Suluhu akiapa kuwa ataitii Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Rais John Pombe Magufuli akitia saini kitabu cha utii.Katika siku ya kihistoria nchini Tanzania
ambapo , Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi nchi ikiwa na Amani na Utulivu baada ya kupigiwa mizinga 21,kukagua gwaride la Jeshi la Wananchi wa Tanzania akiamini  ameiacha nchi katika mikono salama ya Dkt John Pombe Magufuli.Na makamu wake Samia Suluhu Hassani.
Rais Magufuli na makamu wake Mhe.Suluhu wameapa mbele ya Jaji Mkuu wa watanzania Mhe. Othman Chande ,Rais anayeachia madaraka na Makamu wake,Spika wa Bunge Mhe.Anne Makunda pamoja na viongozi wa dini.
Baada ya kuapishwa viongozi wa madhehebu ya Dini walisoma Dua zao,kumshukuru Mungu kwa mafanikio makubwa yaliyo patikana ya kumpata Rais ambaye atalipeleka Taifa hilo mbele.
Aidha Rais Magufuli katika hotuba yake fupi amemshukuru Rais mstaafu Dkt Kikwete,pamoja na viongozi wote na makada wa Chama chake kwa kumpendekeza aingie kwenye kugombea nafasi hiyo na Leo ndoto yake imekamilika ya Kutinga Ikulu.Akiwa na kauli mbiu yake Hapa ni Kazi Tu.Na kwamba leo  ilikuwa ni siku ya kutoa shukrani tu siyo hotuba.
Ameishikuru Tume ya Uchaguzi,wananchi wote kwa kuendesha shughuli za Uchaguzi kupita kwa Amani na Utulivu.Utulivu huo mndiyo uliyo Ingiza Tanzania kwa mara ya kwanza kuwa na Makamu wa Rais Mwanamke Mheshimiwa Samia  Hassani Suluhu.
Maapisho hayo yamefanyika mbele  ya umati wa wananchi wa Dar es Salaam huku mvua ikinyesha za rasharasha lakini walivumilia kushuhudia Rais wa Mabadilko anaapishwa,ikiwa ni pamoja na Marais mbalimbali wa Nchi za Kiafrika  na Nchi Rafiki Duniani wame jionea wenyewe jinsi kisiwa cha Amani kinavyo achiana Madaraka kwa ngazi ya Urais kwa Amani kubwa.
Baadhi ya nchi hizo ni pamoja na Zimbabwe,Afrika Kusini,Kongo,Malawi,Kenya ,Uganda, Zambia,Ethiopia,Bowasna,Namibia,Algeria,Komoro,Nigeria,Madagasca,Angola,Ghana.
Nyingine ni pamoja na Nchi za Falme za Kiarabu,Marekani, Uingereza, Ufransa,Uholanzi,Japani,Denmark,Norywo,Sedeni,Visiwa vya Shelisheli, Umoja wan chi za Ulaya,Jumuiya ya Umoja wa Afrika Mashariki,SADEC .
Katika sherehe hizo zilipambwa kwa  Gwaride,ngoma,kwaya ,Sarakasi na Yamoto Bendi iliyo kamilisha burudani na shughulu hizo uwanjani hapo.