Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Kassim akiapa katika viwanja vya Ikulu ndogo Chamwino nje ya mji wa Dodoma leo saa 4.asubuhi.
Mhe. Majaliwa akimshukuru Rais na wabunge wenzake baada ya kuthibitishwa na wabunge wenzake hapo jana.
Dkt Magufuli
ametaja baadhi ya kero hizo ni pamoja na Rushwa na ufisadi ambao unafanywa na
baadhi ya watu waliopewa dhamana ya kuwahudumia wananchi katika sekta za
Ardhi,Bandari,TAMISEMI, Maji safi na salama,TRA, TANESCO, na Afya kuwa na lugha chafu kwa wagonjwa pamoja na madawa kutokuwepo katika hospitali.
Kero
nyingine ni pamoja na Ajira,Elimu,Vyombo ya usalama ,Polisi,mizani ya
magari,Mahakam,Migodi hasa wachimbaji wadogo wadogo,madeni,kilimo, uvuvi na
ufugaji pamoja na uchakavu wa miundo mbinu na ujenzi wa Reli za zamani na mpya.
Aidha
alisema kuwa Serikali yake ya Awamu ya tano kuwa itatekelza ahadi zote zilizo
ahidiwa za kuwa letea wananchi maendeleo kwa kujenga na kufufua viwanda na wale ambao hawviendelezi serikali
itavichukua.na kwamba kupitia Sekta binafsi inakuwa ni msingi imara ya kuleta
maendeleo.
Alisema
serikali hiyo itaimarisha ufuatiliaji,kilimo,mifugo na uvuvi,Viwanda vitapata
mali ghafi kutoka ndani kwenye viwanda vya nguo ,mafuta,viatu.ili mafanikio
katika kilimo wakulima wapatiwe zana za kisasa,kukopeshwa pamoja na kuondoa
kodi katika mazao
Pia alisema
kuwa akina mama lishe,bodaboda,wachimbaji wadogo wadogo wanufaike na
Halmashauri,Wilaya, Mkoa kwa ushirikiano wao waondoe ushuru usiyo na sababu ili
kuwa na ajira yao ya uhakika.
Katika
kutekeleza ahadi zake Rais huyo amesema ataunda Mahakama ya Mafisadi na
Rushwa,kwa chukizwa na rushwa na ufisadi amefananisha na mtumbua majipu.Ameomba
ushirikiano kwa wabunge na wananchi afanye kazi ya kutumbua majipu hayo
Sambamba na
hayo Rais amesitisha safari zote za nje ya nchi zikiwamo za mafunzo,badala yake
ni rahisi kumwalika mkufunzi mmoja wa mafunzo hayo kuja kutoa mafunzo hapahapa
nchini ili kuokoa fedha ambazo zingeweza kufanyia maendeleo katika Sekta za
kijamii.
Amesema kuna
watu wanapenda kusafiri kwenda nje kuliko kwenda kwao kusalimia wazazi wao
,ambapo kwa mwaka 2013/2014 safari za nje ya nchi zimegharimu shilingi Bilioni
356.324 ikiwa Gharama ya ticket ni billion 183.16,mafunzo billion 68.612 na
posho shilingi bilioni.104.552 .
Waliotumia
fedha hizo ni pamoja na Bunge,TAMISEMI,Mambo ya nje,fedha,ukaguzi na mambo
mengine, hasa hasa anasisitiza uwajibikaji katika kubana matumizi ya fedha na
hizo pesa zinazokusanywa zitumike kwa
maendeleo ya nchi.Kutokana na hayo alisema kuwa kuanzia januari 2016 elimu ni
bure kutoaka Awali hadi Sekondari.
Kuona Rais
huyo kuona umuhimu wa wananchi wake wanopata shida katika Sekta ya afya amesema
fedha kiasi zaidi ya shilingi 230,000,000 rilizo kusanywa na wadau
mablimbali katika viwanja vya Bunge
Mjini Dodoma kwenye hafla fupi aliyo iandaa Rais zielekezwe kununulua vitanda vya hospitali
Na katika
hotuba yake alifungua bunge la 11,ambapo Waziri Mkuu Majiliwa Kassim Majaliwa
aliahirisha bune hilo hadi tarehe 26 Januari 2016,baada ya hotuba fupi kwa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Aidha ali
ahidi kushirikiana na wabunge wote bila kujali Itikadi za Vyama baada ya
hushuhudia wabunge wa Kambi ya upinzani kukaidi amri ya Spika wa Bunge Mhe. Job
Ndugai na kuwa toa nje ya Bunge,si kitendo kizuri kwa wananchi walio wachagua
kwenda kuwa wawakilisha
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni