Alhamisi, 5 Novemba 2015

DKT. JOHN JOSEPH POMBE MAGUFULI AAPISHWA RASMI KUWA RAIS WA AWAMU YA TANO WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA MAKAMU WAKE MHE.SAMIA HASSAN SULUH NA JAJI MKUU WA TANZANIA MHE. OTHMAN CHANDE KATIKA UWANJA WA UHURU JIJINI DAR ES SALAAM,NA KUWASHUKURU WOTE WALIYO FANIKISHA KUWA RAIS

 Rais Mteule Dkt John Josehp Pombe Magufulu akiapa mbele ya Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe.Othman Chande katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dar es Salaam leo
 Makmu wa Rais Mhe. Samia Hassan Suluhu akiapa kuwa ataitii Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Rais John Pombe Magufuli akitia saini kitabu cha utii.Katika siku ya kihistoria nchini Tanzania
ambapo , Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi nchi ikiwa na Amani na Utulivu baada ya kupigiwa mizinga 21,kukagua gwaride la Jeshi la Wananchi wa Tanzania akiamini  ameiacha nchi katika mikono salama ya Dkt John Pombe Magufuli.Na makamu wake Samia Suluhu Hassani.
Rais Magufuli na makamu wake Mhe.Suluhu wameapa mbele ya Jaji Mkuu wa watanzania Mhe. Othman Chande ,Rais anayeachia madaraka na Makamu wake,Spika wa Bunge Mhe.Anne Makunda pamoja na viongozi wa dini.
Baada ya kuapishwa viongozi wa madhehebu ya Dini walisoma Dua zao,kumshukuru Mungu kwa mafanikio makubwa yaliyo patikana ya kumpata Rais ambaye atalipeleka Taifa hilo mbele.
Aidha Rais Magufuli katika hotuba yake fupi amemshukuru Rais mstaafu Dkt Kikwete,pamoja na viongozi wote na makada wa Chama chake kwa kumpendekeza aingie kwenye kugombea nafasi hiyo na Leo ndoto yake imekamilika ya Kutinga Ikulu.Akiwa na kauli mbiu yake Hapa ni Kazi Tu.Na kwamba leo  ilikuwa ni siku ya kutoa shukrani tu siyo hotuba.
Ameishikuru Tume ya Uchaguzi,wananchi wote kwa kuendesha shughuli za Uchaguzi kupita kwa Amani na Utulivu.Utulivu huo mndiyo uliyo Ingiza Tanzania kwa mara ya kwanza kuwa na Makamu wa Rais Mwanamke Mheshimiwa Samia  Hassani Suluhu.
Maapisho hayo yamefanyika mbele  ya umati wa wananchi wa Dar es Salaam huku mvua ikinyesha za rasharasha lakini walivumilia kushuhudia Rais wa Mabadilko anaapishwa,ikiwa ni pamoja na Marais mbalimbali wa Nchi za Kiafrika  na Nchi Rafiki Duniani wame jionea wenyewe jinsi kisiwa cha Amani kinavyo achiana Madaraka kwa ngazi ya Urais kwa Amani kubwa.
Baadhi ya nchi hizo ni pamoja na Zimbabwe,Afrika Kusini,Kongo,Malawi,Kenya ,Uganda, Zambia,Ethiopia,Bowasna,Namibia,Algeria,Komoro,Nigeria,Madagasca,Angola,Ghana.
Nyingine ni pamoja na Nchi za Falme za Kiarabu,Marekani, Uingereza, Ufransa,Uholanzi,Japani,Denmark,Norywo,Sedeni,Visiwa vya Shelisheli, Umoja wan chi za Ulaya,Jumuiya ya Umoja wa Afrika Mashariki,SADEC .
Katika sherehe hizo zilipambwa kwa  Gwaride,ngoma,kwaya ,Sarakasi na Yamoto Bendi iliyo kamilisha burudani na shughulu hizo uwanjani hapo.  

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni