Alhamisi, 19 Novemba 2015

MHESHIMIWA MAJALIWA KASSIM MAJALIWA ATHIBITISHWA KUWA WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WA AWAMU YA TANAO KWA ASILIMIA 73.5 KWA KURA 258 BAADA YA KUPIGIWA KURA NA WABUNGE WOTE LILIPO PELEKWA BUNGENI JINA LAKE KWA STAHILI YA AINA YAKE KUTOKA KWA RAIS.


Mheshimiwa Majiliwa amesemwa kuwa ni mtu, Mwadilifu,asiye na makundi, hana kashfa, mtetezi, mfuatiliaji, makini,msikivu, mwenye busara,ni mchapa kazi,kujichanganya na watu na mwana michezo,na kwamba ni kijana ambaye atatekeleza vyema moto wa hapa kazi tu kwaushirikiano na Rais ,wabunge wenzake pamoja na wananchi.
Majaliwa ni Waziri Mkuu kijana kati ya mawaziri wakuu wa Awamu zote ,aidha amewahi kufanya kazi mbalimbali zikiwemo kwenye Sekta ya elimu, akiwa mwalimu, Mkufunzi katika vyuo vya Ualimu, Katibu wa Chama Cha Walimu Tanzania, Mkuu wa Wilaya ,Naibu Waziri wa Elimu TAMISEMI.Akaibuka kwa kura 258 sawa na asilimia73.5
Kutokana na nafasi aliyokuwa nayo TAMISEMI na nyingine zote alizozifanya katika  Utumishi wake ,inasemakana ana upeo mkubwa wa kutekeleza majukumu yake kama Waziri Mkuu kwa kuwa anayaelewa vizuri maeneo yake atakayo yafanyia kazi bila mashaka yoyote. Kesho saa 4. Asubuhi ataapishwa katika viwanja vya Ikulu ndogo Chamwino Mjini Dodoma.
Hatimaye  Dkt Tulia ckson Mwansasu  akaibuka kuwa mshindi wa kiti cha Unaibu Spika kwa asilimia 71.2 sawa na kura 250 alizopata baada ya kumshinda Mhe.Magdalena Sakaya wa  CUF Kaliua Tabora aliyepata kura 101 sawa na asilimia 28.8.,nakwamba Dkt Mwansasu akaapishwa kuwa Naibu Spika wa Bunge la 11.
Hii ni Serikali ya kihistoria nchini Tanzania kuwa  na Rais  na Makamu wake mwanamke Mhe.Samia Suluhu Hassan na Naibu Sipika Bunge la Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania mwanamke Dkt Tulia Ackson Mwansasu. Kweli hapa ni kazi tu.kinacho hitajika ni ushirikiano kutoka kwa wananchi  wote.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni