Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akisalimiana na Mabalozi pamoja na Wafanya biashara katika ukumbi wa Ikulu Jijini Dar es Salaam leo.
JUMUIYA YA WAFANYA
BIASHARA NA MABALOZI WANAO WAKILISHA NCHI ZAO NA WANANCHI WENGINE WAMECHANGA BILIONI 1 MILIONI 366 KUFUATIA TETEMEKO LA KAGERA
Hayo yametokana na wito wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa kukutana na Jumuiya ya wafanya
biashara na Mabalozi wanao wakilisha nchizao Nchini Tanzania na wananchi
wengine kutoa michango yao ya hali na mali kufuatia tetemeko kubwa lililotokea tarehe 10/ 09 / 2016 , lenye Tani 7.7 ambalo limeua watu 17,majeruhi 253 ambapo
watu 143 wamelazwa hosipitali wakiendelea na matibabu.
Kufuatia wito huo fedha zimepatikana shilingi Bilioni 1 ,mbili
za 366, ikifuatiwa na Makampuni matatu
ya mafuta yame ahidi kujenga sekondari
za Nyakato na Ihungo
Waziri wa Viwanda na Uwekezaji Mhe. Charles John Mwijage amesema
mwananchi yeyote aliyeguswa na tukio
hilo achangie,maana tatizo ni kubwa.Aidha amewashukuru wote waliyo kubali
kushiriki katika kikao hicho cha kumuunga mkono Waziri Mkuu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni