Ijumaa, 30 Septemba 2016

MGENI RASMI BWANA EMANUEL PIUS MUSHI WA IPAGALA MANISPAA YA DODOMA ATOA MIFUKO 10 YA SARUJI KUONGEZA MATUNDU YA VYOO SHULE YA MSINGI MAKOLE MANISPAA YA DODOMA.






.MFUKO WA SUKARI.
.MFUKO WA UNGA WA NGANO.KWA AJILI YA CHAI YA WALIMU ,
.NA BAHASHA KWA WALIMU WA DARASA LA SABA
Bwana Mushi alisema hayo kwenye mahafali ya darasa la saba 149 Wavulana 66 na wasichana 83 yaliyofanyika katika shule ya msingi ya Makole Manispaa ya Dodoma  leo.
Alisema kuwa walimu ni watu muhimu sana katika kuinua elimu,kulea watoto kinidhamu pamoja na kuwafanya wawe wananchi wema wa kuijenga taifa la Tanzania.
Katika kujibu Risala ya wanafunzi kuhusu changamoto zinaziikibili shulie hiyo ,zikiwemo upungufu wa matundu ya vyoo, ukoesefu wa meza na viti vya walimu shuleni hapo,ameahidi kukabili changamoto zikiwemo pamoja .
Na kutoa mifuko 10 ya saruji, Meza 2 na viti vyake,na kwamba atatoa pia mfuko moja wa kilo 25 za sukari, mfuko wa unga wa ngano kwa ajili ya chai ya walimu .
Aidha mgeni rasmi huyo ametoa motisha kwa walimu wanaofundisha darasa la saba kwa juhudi kubwa waliyo ifanya kufanikisha uelemishaji wa  vijana waliyo hitimu elimu ya msingi na kusubili kuendelea na masomo au kuingiakwenye uwanja wa mapambano ya maisha.
Bwana Mushi amewauliza wazazi wa watoto waliyo maliza elimu ya msingi kuwa ni wangapi wapo tayari kuongeza nguvu katika kukabiliana na changamoto za shule hizo, hakukuwepo hata mzazi mmoja aliyesema yuko tayari.
Akasema yeye akasema yuko tayari kuanzia juma tatu ijayo atakuwa bega kwa bega na kamati ya shule katika kuhakikisha ujenzi wa vyoo hivo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni