Ijumaa, 30 Septemba 2016

WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KASSIMU MAJALIWA HAMIA RASMI LEO DODOMA

Mheshinmiwa Majaliwa ametua na ndege katika uwanja wa ndege wa Dodoma majira ya Jioni yeye na familia yake,kukamilisha ahadi yake ya kuhamia hapa mwezi wa 9 mwaka huu.
Katika Sikukuu ya Mashujaa iliyoazimishwa kwenye viwanja vya mashujaa Mjini Dodoma Waziri Mkuu alisema nyumba yake ikikamilika kule mlimani atahamia,na kweli leo ametimiza ahadi yake ya kuhamia Makao makuu ya Chama na Serikali Dodoma ndiyo kwenyewe.

MGENI RASMI BWANA EMANUEL PIUS MUSHI WA IPAGALA MANISPAA YA DODOMA ATOA MIFUKO 10 YA SARUJI KUONGEZA MATUNDU YA VYOO SHULE YA MSINGI MAKOLE MANISPAA YA DODOMA.






.MFUKO WA SUKARI.
.MFUKO WA UNGA WA NGANO.KWA AJILI YA CHAI YA WALIMU ,
.NA BAHASHA KWA WALIMU WA DARASA LA SABA
Bwana Mushi alisema hayo kwenye mahafali ya darasa la saba 149 Wavulana 66 na wasichana 83 yaliyofanyika katika shule ya msingi ya Makole Manispaa ya Dodoma  leo.
Alisema kuwa walimu ni watu muhimu sana katika kuinua elimu,kulea watoto kinidhamu pamoja na kuwafanya wawe wananchi wema wa kuijenga taifa la Tanzania.
Katika kujibu Risala ya wanafunzi kuhusu changamoto zinaziikibili shulie hiyo ,zikiwemo upungufu wa matundu ya vyoo, ukoesefu wa meza na viti vya walimu shuleni hapo,ameahidi kukabili changamoto zikiwemo pamoja .
Na kutoa mifuko 10 ya saruji, Meza 2 na viti vyake,na kwamba atatoa pia mfuko moja wa kilo 25 za sukari, mfuko wa unga wa ngano kwa ajili ya chai ya walimu .
Aidha mgeni rasmi huyo ametoa motisha kwa walimu wanaofundisha darasa la saba kwa juhudi kubwa waliyo ifanya kufanikisha uelemishaji wa  vijana waliyo hitimu elimu ya msingi na kusubili kuendelea na masomo au kuingiakwenye uwanja wa mapambano ya maisha.
Bwana Mushi amewauliza wazazi wa watoto waliyo maliza elimu ya msingi kuwa ni wangapi wapo tayari kuongeza nguvu katika kukabiliana na changamoto za shule hizo, hakukuwepo hata mzazi mmoja aliyesema yuko tayari.
Akasema yeye akasema yuko tayari kuanzia juma tatu ijayo atakuwa bega kwa bega na kamati ya shule katika kuhakikisha ujenzi wa vyoo hivo.

Jumanne, 13 Septemba 2016

BILIONI 1 MILIONI 366 ,NA SHULE MBILI ZA SEKONDARI KUFUATIA ATHARI ZA TETEMEKO LA KAGERA

 Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles John Mwijage akiongea na Wafanya biashara,na Mabalozi wanao wakilisha nchi zao Tanzania kumuunga mkono Waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa katika Ukimbi wa Ikulu Jijini Dar es Salaam leo.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akisalimiana na Mabalozi pamoja na Wafanya biashara katika ukumbi wa Ikulu Jijini Dar es Salaam leo.



JUMUIYA YA WAFANYA BIASHARA NA MABALOZI WANAO WAKILISHA NCHI ZAO NA WANANCHI WENGINE  WAMECHANGA BILIONI 1 MILIONI 366 KUFUATIA TETEMEKO LA KAGERA

Hayo yametokana na wito wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa kukutana na Jumuiya ya wafanya biashara na Mabalozi wanao wakilisha nchizao Nchini Tanzania na wananchi wengine kutoa michango yao ya hali na mali kufuatia tetemeko kubwa lililotokea  tarehe 10/ 09 / 2016 , lenye Tani  7.7 ambalo limeua watu 17,majeruhi 253 ambapo watu 143 wamelazwa hosipitali wakiendelea na matibabu.

Kufuatia wito huo fedha zimepatikana shilingi Bilioni 1 ,mbili za  366, ikifuatiwa na Makampuni matatu ya mafuta yame ahidi kujenga sekondari     za Nyakato na Ihungo

Waziri wa Viwanda na Uwekezaji Mhe. Charles  John Mwijage amesema mwananchi yeyote aliyeguswa na  tukio hilo achangie,maana tatizo ni kubwa.Aidha amewashukuru wote waliyo kubali kushiriki katika kikao hicho cha kumuunga mkono Waziri Mkuu.

Jumapili, 11 Septemba 2016

CHUMVI IKIKOSA LADHA HAIFAI KWA MATUMIZI YA BINADAMU,MASHAMASI WAMETAHARISHWA WASIGEUKE KUWA CHUMVI ISIYOYEYUKA

 Askofu mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es salaam Cardnari Policap Pengo,amewaambia Mashemasi wawili waliyo pata Daraja la Ukuhani na Maendeleo ya Kanisa la Kristu Ushemasi katikaKipindi cha Kutoka Kanisani  na TBC ,kuwa wasiwe chumvi mawe.Amesema watakiwa wawe chumvi kwa ajili ya watu na siyo kwa binafsi zao.
 Mashemasi Peter Mbula Mwana na mwenzake baada ya kupata daraja hilo la Ushemasi
Misa Takatifu imesomwa na Padre katika Picha.

Jumamosi, 10 Septemba 2016

TIMU ZA VETERANI ZA TUNDUMA NA DODOMA VETERANI ZA TOKA SARE YA 2-2 KATIKA UWANJA WA JAMHURI MJINI DODOMA

 Timu za Veterani  za Tunduma Mbeya na Dodoma zikimenyana katika uwanja wa jamhuri Mjini Dodoma
Timu hizo zime toka sare ya magoli mawili

Timu ya Veterani ya Tunduma kutoka Mkoa wa Mbeya  wameteoka sare ya magoli mawili kwa mawili na Timu ya Veterani ya Mkoa wa Dodoma leo.
Katika kipindi cha dakika 30 za kwanza Tunduma ilianza kuliona lango la Veterani ya Dodoma  golo lililofungwa kwa peneti na Alex Kamugisha,mchezo ukawa mkali katika dakika za mwisho za kindi cha kwanza Alex kamugisha alifunga goli la pili.Mpaka kipenga kilipopogwa ikilikuwa Tunduma 2 na Dodoma Veterani bila.
Katika kipindi cha pili haliya hewa iligeukia Dodoma Veterani ambapo  Weston Wanjala aliipatia Dodoma goli la kwanza ,fumba na kufumbua  Frenk Wana alifunga goli la pili na kufanya sare ya Tunduma 2 na Dodoma 2





Ijumaa, 19 Agosti 2016

OFISI ZA WIZARA MBALIMBALI KATIKA SERIKALI KUHAMIA DODOMA ZIMEKAMILIKA KWA ASILIMIA SABINI { 70 ] NA NYUMBA ZA WATUMISHI KWA ASILIMIA SABINI NA TANO { 75 }

Ambapo balozi wa China na Kuwet wapo tayari kuhamia Dodoma na kwamba wapo tayari kujenga majengo ya Ofisi za Ubalozi wao.
Serikali katika suala la kuhamia Dodoma siyo la Kurupuka,bali ni suala la muda mrefu tangu mwaka 1973 maazimio yaliyo jadiliwa kwenye mkutano wa TANU.
Aidha Serikali imejipanaga kujenga reli ya kati ,michoro tayari kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam Trani ya mwendo kasi,upanuzi wa uwanja wa dege utakaoweza kutua ndege kubwa na ndogo, pamoja na bandari kavu.Hizo ni dalili  ya maandalizi ya kuwa na Jiji kutoa fursa mbalimbali za wawekezaji wakubwa na wadogo,na wajasiliamali. [ KARIBUNI DODOMA]
Hayo yamesemwa na Waziri mwenye dhamana, Mhe. Jenista Mhagama Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge,Kazi,Vijana na Walemavu katika Kipindi cha KUHAMIA DODOMA kinacho rushwa na TBC.Jumatano.

Jumamosi, 30 Julai 2016

TUWEKE MASILAHI YA WANANCHI KWANZA ,VYAMA BAADAYE - MAGUFULI

Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli,akiongea na wananchi wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida, awatoa wasiwasi wananchi kuwa tatizo la sukari litaisha siku zijazo na kwamba sukuri itashuka bei kwani kuna baadhi ya watu watajenga viwanda vya sukari.
 Wafanya biashara wababaishaji wanaoficha vitu atawashughulikia ,pia asema  changamoto hizi niza muda tu maisha yatakwenda watu wote  na kwa vyama vyote.
Aidha alisema kuwa yeye hajaribiwi, na hatajaribiwa na mtu yeyote katika uongozi wake, awataka wananchi kufanya kazi kwa maendeleo yao, asema yuko pamoja na wananchi waliyo mchagua na hata waangusha kamwe.

TANZANIA INA VIVUTIO VINGI VIKIWEMO,HIFADHI ZA TAIFA,NA WANYAMA PORI

 Tembo na mnyama  mkubwa ila wanaonewa kwa kung'olewa pembe zao na watu wanataka utajiri wa harakaharaka.
Twiga ni mnyama mpole sana,yupo Tanzania

DODOMA LEO,DODOMA AMBAYO WIZARA ZA SEIKALI YA AWAMU YA TANO INAMIA MAKAO MAKUU YA CHAMA

Huo ni mzunguko wa Dodoma kutokea Bungeni,Kuelekea Mji wa Dodoma , na hapo Stendi ya mabasi yatokayo mikoani na yaendayo Dar es Salaama

Jumatano, 27 Julai 2016

WAZIRI WA NCHI OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA, WAZEE NA WALEMAVU KUHAMIA DODOMA WIKI LA KWANZA LA MWEZI WA NANE MWAKA HUU

Mhe. Jenista Joackim Mhagama,akiongea na watendaji wa TAMISEMI Jijini Dar es Salaam, kuwa wakati ofisi yake na Manaibu waziri wake hawajahamishia Dodoma ofisi zao, Mapema mwezi wa Nane mwaka huu,watendaji hao wawe wakwanza kuhamia huko ili wawapokee.

Kama wao watakavyo Mpokea Waziri Mkuu atakapo hamia Dodoma mwezi wa Tisa,kama alivyo muhaidi Rais kuwa suala la kuhamia Dodoma atalifanyia kazi,kwa kuwa wakanza kuhamia Dodoma mwezi wa tisa mwaka huu.

Alisema iwepo kuna baadhi yao wana nyumba Jijini ni vyema wazipangishe nyumba hizo.Na kwamba iwapo kama kuna makatibu wakuu walipanga bajeti zao kwa ajili ya ujenzi,basi majengo hayo yakajengwe Dodoma

Jumatatu, 25 Julai 2016

NYUMBA YANGU IKIKAMLIKA MWEZI WA 9 MWAKA HUU NAHAMIA DODOMA – MAJALIWA



WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa kassim,ametamka rasmi kwa mawaziri na Makatibu wakuu kuhamia Dodoma mara moja.

Alisema hayo alipokuwa akiwasalimia wananchi waliyo hudhuria katika viwanja vya mashujaa mjini Dodoma kwenye kilele cha kumbukumbu za mashujaa leo,na kwamba wawekezaji wajipange katika kuwekeza Dodoma.

Alisema watu wajenge mahoteli  ya kitalii makubwa,nyumba za kulala wageni, nyumba za kuishi na   kwa kuwa mji utakuwa na watu wengi ambao watahitaji mahitaji yao.kuandaa mazingira ya kupokea wageni mbalimbali wakiwemo mabalozi.” Hiyo ndiyo fursa ya uwekezaji, hivyo tumieni fursa hizo.” Alisema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.