Jumatatu, 25 Julai 2016

NYUMBA YANGU IKIKAMLIKA MWEZI WA 9 MWAKA HUU NAHAMIA DODOMA – MAJALIWA



WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa kassim,ametamka rasmi kwa mawaziri na Makatibu wakuu kuhamia Dodoma mara moja.

Alisema hayo alipokuwa akiwasalimia wananchi waliyo hudhuria katika viwanja vya mashujaa mjini Dodoma kwenye kilele cha kumbukumbu za mashujaa leo,na kwamba wawekezaji wajipange katika kuwekeza Dodoma.

Alisema watu wajenge mahoteli  ya kitalii makubwa,nyumba za kulala wageni, nyumba za kuishi na   kwa kuwa mji utakuwa na watu wengi ambao watahitaji mahitaji yao.kuandaa mazingira ya kupokea wageni mbalimbali wakiwemo mabalozi.” Hiyo ndiyo fursa ya uwekezaji, hivyo tumieni fursa hizo.” Alisema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni