Jumatatu, 25 Julai 2016

MAGUFULI AWATAKA WATANZANIA KUDUMISHA AMANI NA UTULIVU

 Amiri Jeshi wa Majeshi yote ya Ulinzi na Usalama Dkt. John Magufuli alisema watanzania tuwaenzi mashujaa waliyo poteza uhai wao kwa ajili ya kutetea Amani ya nchi yetu.

 Baadhi ya wananchi wakishuhudia kumbukumbu za mashujaa katika viwanja vya mashujaa Dodoma


Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ,amesema ni wa wajibu wao kudumisha amani,kwani amani ikitoweka haiwezi kurudi,wananchi wamepigania nchi hii hata kupoteza uhai  wao kwa ajili ya Taifa lao,askari wamepoteza maisha yao kwa ajili ya taifa lao,hivyo amani hiyo  tuilinde.
    Hayo yamesemwa na Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dkt John Magufuli  baada ya kuweka mkuki na ngao kwenye mnara wa kumbukumbu ya mashujaa  katika viwanja vya mashujaa mjini Dodoma leo,na kwamba mashujaa hao waliyo toa uhai wao ,walitoa kwa ajili ya Taifa bila kujali kabila,dini,au vyama vyao.
   Aidha amerudia tena ahadi yake ya kuhamia Dodoma ndani ya miaka minne na miezi minne iliyo bakia,” ikiwa zaidi ya Wabunge 300 na ofisi za mawaziri zipo Dodoma kwa nini makao Makuu ya nchi yasihamie Dodoma” Alisema Magufuli.
   Watanzania wakahubili Amani,kila mmoja akahubili amani,anataka watanzania wamwombee ili aipeleke Tanzania anakotaka ifike,hata kila mtu aseme ameiacha Tanzania ina Amani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni