Jumamosi, 23 Julai 2016

KABLA YA KUMALIZA MIAKA MITANO YA UONGOZI WAKE, SERIKALI ITAHAMIA DODOMA – MAGUFULI

 Mwenyekiti wa awamu ya Tano Dkt.John Pombe Magufuli akihutubia wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM katika Ukumbi wa CCM nje kidogo ya Mji wa Dodoma leo.Ambapo amewashukuru sana  baadhi ya viongozi wakiwemo Rais Mstaafu Ally Hassan Mwinyi, Wiliam Benjamini Mkapa na Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete waliyomfanya afikie katika wadhifa wake.
 Jukwaa kuu la Viongozi wa CCM wakisubiri wajumbe wakimpigia kura Dkt John Magufuli,ambapo matokeo yalikuwa kura 2,398 za ndiyo ambopo kura za hapana hazikuwepo na zilizoharibika pia hazikuwepo.
 Mwenyekiti Mtaafu Dkt Jakaya Kikwete akimkabidhi vitabu  vinne vya tathimini ya uchaguzi mkuu uliyopita,Dkt.John Pombe Magufuli, leo baada ya kumtangaza kuwa mshindi wa kura zote zilizopigwa na wajumbe wote.
Katibu Mkuu wa CCM Kinana akitoa shukrani zake kwa viongozi wote waliyopita na wasasa aliyofanya kazi nao na kukifikisha Chama hicho katika mafanikio makubwa katika uchaguzi Mkuu uliyopita.na kuahidi kuwa atafanya kazi na Sekreterieti yake kwa uadilifu mkubwa.



KABLA YA KUMALIZA MIAKA MITANO YA UONGOZI  WAKE, SERIKALI ITAHAMIA DODOMA – MAGUFULI
Mwenyekiti wa tano wa Chama cha Mapinduzi Dkt John Pombe Magufuli alisema hayo baada ya kukabidhiwa uwenyekiti na Mwenyekiti Mstaafu Dkt .Jakaya Kikwete katika ukumbi wa CCM Mjini Dodoma leo.
    Alisema Dodoma ni  makao makuu ya Chama Cha Mapinduzi  {CCM},ina chuo kikuu kizuri, ina Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Muungano,Na sherehe  za Mashujaa zitafanyika tarehe 25 Julai 2016.kwa nini Serikali yake isihamie Dodoma.
   Aidha alisema kuwa Mwalimu Nyerere aliposema Dodoma ni makao makuu ya Chama  hakufanya masihala ila alikuwa anaimanisha kweli kabisa.
    Awali wajumbe wa Chama hicho walipigia kura ya Dkt Johan Pombe Magufuli kura ,ambapo kura zilizo haribika hakuna,kura za hapana hazikuwepo na kura za ndiyo zilikuwa 2,398. Na kukabidhiwa vitendea kazi katika Chama. Na Kuelezea jinsi atakavyo fanya kazi kwa uadilifu kwa kuwa yumo ndani ya Chama hicho kwa miaka 40.
    Alisema kuwa atafanya kazi kwa ushirikiana na wanachana wenzake kwa uaminifu  kwa kumtanguliza Mungu katika kutokomeza Rushwa ndani ya Chama ambapo chama hicho kina uwezaekano mkubwa wa kutoa na kupokea rushwa katika kutafuta madaraka.
    Amewahakikishia kuwa iwapo kuna watu ambao waliyozoewea kupata vyeo kwa rushwa  hana nafasi katika uongozi wake kama yupo ajitowe mwenyewe ,na kwamba kama kuna majipu ndani ya Chama atayatumbua kwelikweli.
   Vilevile amewaambia wajumbe hao kuwa baadhi ya haadi alizozitoa wakati wa kuomba ridhaa kwa wananchi ya kuomba kupeperusha bendera ya  CCM ametimiza, zikiwemo Elimu bure, Bomba la mafuta kutoka Uganda,Reli ya kati kukarabatiwa shilingi Rrioni moja imeandaliwa kwa shughuli hizo.
   Mwenye kiti huyo aliwashukuru wote waliyo mfanya awe Rais na kuwa Mwenyekiti wa tano wa Chama hicho.
   Kabla ya kuhitimisha hotuba yake Magufuli alisoma barua iliyoa andikwa na katibu Mkuu wa CCM kwa niaba ya Sekreterieti ya CCM,na kuijibu kuwa waendelee  na madaraka yaou mpaka hapo itakapokwa ina faa kufanya vinginevyo.  

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni